Boeing 737 yaanguka wakati ikipaa Senegal

0
490

Ndege aina ya Boeing 737-300 imeanguka wakati ikipaa nchini Senegal na kujeruhi watu 11, wanne kati yao vibaya.

Ndege hiyo ya Air Senegal HC 301 iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Mali, Bamako ilitoka kwenye njia ya kurukia ndege mapema leo, katika kiwanja cha ndege cha Dakar cha Blaise Diagne, imesema taarifa.

Rubani alijeruhiwa kidogo, lakini idadi kubwa ya abiria 78 waliokuwemo hawakujeruhiwa katika tukio hilo.

Shughuli zimesitishwa katika kiwanja hicho cha ndege huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini sababu za tukio hilo.