Rolls-Royce imeingiza sokoni aina nyingine ya pili ya magari yake ya Cullinan (Cullinan Series II) ambayo ni mageuzi mapya na makubwa katika uundaji wa magari ya kifahari yaliyochupa juu (SUV). Aina hii ya magari, Cullinan Il inahusisha matumizi ya hali ya juu ya kidijiti na inaonesha muundo mpya wa ndani ya gari unaotumia vitu/vifaa vya kuvutia kwelikweli.
Gari hili, Cullinan Il, linajibu mabadiliko ya mahitaji ya wateja wa Rolls-Royce ambao wanapenda vitu babu kubwa na vyenye starehe ya hali ya juu.
Miongoni mwa magri ya Rolls-Royce, Cullinan inabaki kuwa mojawapo ya magari bora kabisa kuzalishwa na kampuni na ingizo jipya la Cullinan Il linatoa taswira kwamba Rolls-Royce itaendelea kuongoza kwa magari yaliyopanda juu (SUV).