Miaka 62 ya Red Cross katika jamii

0
164

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki katika maadhimisho ya miaka 62 ya kazi ya kuhudumia watanzania inayofanywa na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS), yatakayofanyika Mei 11, 2024 mkoani Dodoma.

Siku hiyo pia itatumika kutambua kazi kubwa inayofanywa na Shirika la Msalaba Mwekundu hapa nchini.

Katibu Mkuu wa
TRCS Lucia Pande amesema zaidi ya wanachama laki nane wa shirika hilo na wale wa kujitolea wamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hasa kwenye maeneo yanayokumbwa na majanga mbalimbali nchini.

Kwa sasa timu za Wataalam wa Shirika hilo la Msalaba Mwekundu zipo kwenye maeneo ya Kusini mwa Tanzania kutoa msaada kwa watu waliokumbwa na kimbunga Hidaya lakini pia Hanang mkoani Manyara ambapo kulitokea maafa ya maporomoko ya tope.