Mwandishi wa habari kwa picha Sebastião Salgado na mke wake Lélia Deluiz Wanick wa nchini Brazil, wamefanikiwa kurejesha msitu wa ekari 1,500 ambao ulikuwa umeharibiwa kutokana na ukataji miti.
Msitu huo ulikuwa ni makao ya zaidi ya aina 500 za mimea na wanyama waliokuwa hatarini kutoweka.
Wenza hao walianzisha mkakati wa kurejesha miti katika msitu huo kwa kuwezesha kuzaliwa upya kwa miti ili kurudisha msitu katika hali yake ya asili kabla ya uharibifu.
Katika kipindi cha miaka 20 walijitolea kupanda miti Milioni mbili jambo ambalo linahitaji juhudi kubwa, kujitolea na uvumilivu mkubwa kwani sio kazi rahisi na hatimaye wakafanikiwa kuufufua msitu na wanyama kurejea katika eneo hilo.
Mafanikio hayo ya Salgado na mke wake Wanick yanaweza kutumika kama mfano wa kuigwa wenye kutia moyo ambao umefanikisha kuonesha namna mwanadamu anaweza kurejesha hali ya asili iliyotoweka katika mazingira yake kutokana na uharibifu wa shughuli za kibinadamu.
Pangusa (swipe) kushoto kuona picha za kabla na baada za msitu huo ulivyokuwa.