Mafua yamkwamisha Rihanna kushiriki Met Gala

0
2351

Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la PEOPLE la nchini Marekani, mwanamuziki na mwanamitindo Robyn Rihanna Fenty (36) maarufu Rihanna au Riri ameshindwa kuhudhuria tamasha la Met Gala kwa mwaka 2024 kutokana na kuugua mafua.

Mashabiki wengi wa Rihanna wameandika mitandaoni wakisema Met Gala bila #Rihanna ni kama haijakamilika kutokana na historia yake ya kutupia viwalo matata katika zulia jekundu wakati wa matamasha ya miaka ya nyuma.

Tamasha la Met Gala kwa mwaka 2024 limefanyika usiku wa Mei 6, 2024 nchini Marekani.