Vyama vije na hoja za kujenga nchi

0
156

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana ametoa rai kwa Watanzania kukataa maneno ya uchonganishi na ya kufarakanisha, kwani ndio njia sahihi ya kuuenzi Muungano na waasisi wake.

Kinana ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa mkutano wake na wanachama wa CCM pamoja na wananchi mbalimbali leo Mei 5, 2024.

Wakati wa mkutano huo Kinana amevitaka vyama vya siasa nchini kuja na hoja zinazojenga nchi na sio kubomoa, kwani hoja pinzani zinarudisha Taifa nyuma na kuharibu dhamira ya kudumisha amani inayoliliwa na Mataifa mengi duniani.

Tupo Mbashara kupitia TBC1, TBC Taifa na mitandao ya kijamii kwa anwani ya TBConline.

📸✍🏾 @simbeyezekiel

TBCDigitalUpdates

ChamaChaMapinduzi