“Kwa sasa hakuna klabu Tanzania inayoweza kuisogelea Young Africans SC kwenye ubora. Ndiyo maana timu nyingi zikicheza na sisi zinakuja na mfumo wa kuzuia zaidi ikimaanisha wanaiheshimu klabu yetu. Malengo yangu makubwa ni kuhakikisha klabu yetu inakuwa moja ya klabu bora.”
“Matamanio yangu ni kuona mwakani kwenye mashindano ya kimataifa tufike katika orodha ya timu nne bora Afrika, ili tuweze kushiriki kombe la dunia la vilabu. Mwaka jana tumefika fainali na tumepata alama nyingi ambazo zitatuongezea nguvu ya kushiriki kombe hilo.”- Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said