Tanzania na Russia kushirikiana kudhibiti uhalifu

0
286

Tanzania imedhamiria kushirikiana na Russia katika kudhibiti uhalifu nchini ukiwemo ule wa kimtandao.

Kushirikiana huko ni pamoja na kuwajengea uwezo askari wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Tanzania kushirikiana na wenzao ambao nchi zao zimeendelea kiteknolojia katika kudhibiti uhalifu huo wa kimtandao unaotajwa kuvuka mipaka.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni katika mkutano wa kimataifa wa maafisa wa ngazi ya juu wanaohusika na mambo ya usalama unaoendelea nchini Russia.

Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki kutoka nchi takribani 20 huku msisitizo ukiwekwa katika kupambana na uhalifu wa kutumia teknolojia ambao umekuwa ni tishio katika mataifa mbalimbali.