Helikopta zagongana na kuua askari 10

0
205

Askari kumi wa Jeshi la Wanamaji la Malaysia wamefariki dunia baada ya helikopta mbili za Jeshi hilo kugongana.

Helikopta hizo zimegongana wakati wa mazoezi ya gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo la Wanamaji nchini Malaysia.

Picha zilizosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zimeonesha helikopta kadhaa zikiruka katika uwanja wa Jeshi la Wanamaji wakati wa mazoez hayo na baadaye mbili kugongana na kusababisha vifo hivyo.