Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji yaomba Bilioni 121

0
151

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ameliomba Bunge likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 yenye jumla ya shilingi Bilioni 121 kwa ajili ya Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na taasisi zake.

Profesa Mkumbo amesema shilingi Bilioni 100 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Bilioni 21 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.