Mkuu wa Majeshi Kenya afariki kwenye ajali

0
262

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Kenya Jenerali
Francis Ogolla amefariki dunia kwenye ajali ya helikopta iliyotokea leo nchimi humo.

Taarifa ya kifo cha Jenerali Ogolla imetolewa kwa Taifa na Rais William Ruto wa Kenya mara baada ya kikao chake na viongozi kadhaa wa nchi hiyo kilichodumu kwa nuda wa saa mbili.

Jenerali Ogolla ni miongoni mwa
Watu tisa waliofariki dunia baada ya helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kuanguka na kuwaka moto katika eneo la Sindar magharibi mwa Pokot.

Taarifa zaidi zinasema watu wengine wawili wamenusurika katika ajali hiyo.