Azam yamwekea Mzize milioni 400 mezani

0
402

Azam FC imewasilisha dau la shilingi milioni 400 kwa Yanga SC ikikusudia kupata saini ya mshambuliaji Clement Mzize.

Azam ambayo kwa sasa haina mshambuliaji baada ya kutofautiana na raia wa Zimbabwe, Prince Dube, inatarajia kumsajili Mzize ambaye mkataba wake na Yanga unaisha Juni 2025.

Wakati hayo yakiendelea, kuna tetesi kuwa Prince Dube ambaye ameweka wazi nia yake ya kuondoka Azam, atajiunga na Yanga kuimarisha safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa kihistoria.

Panda shuka kati ya klabu hizi inaendelea ikikumbukwa kwamba mwaka 2023 mvutano kati yao ulikuwa mkubwa kufuatia kiungo wa Yanga, Fiesal Salum kuamua kuondoka, huku Azam ikidaiwa kuwa nyuma yake, kabla ya baadaye kutangaza kumsajili.