Wavushwa kwa fedha baada ya daraja kujaa maji

0
176

Wakazi wa Kijiji cha Budoda, Kata ya Masumbwe mkoani Geita inawalazimu kulipa shilingi 1,000 ili kuvushwa baada ya daraja katika kijiji chao kufunikwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi George Ruben amekiri kuwepo kwa changamoto ya miundombinu ya barabara kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kwamba watachukua hatua za dharura kunusuru wananchi.