Ngorongoro tumesikia kilio chenu

0
191

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema Serikali imesikia kilo cha Wananchi wa Ngorongoro mkoani Arusha kwa kuboresha matangazo ya redio ya TBC Taifa na Bongo FM.

“Tungetamani sana kuwa na redio inayosikika kila mahali, Waziri ameeleza kuwa usikivu wa hapa ulikuwa hafifu, tulikuwa tunasikiliza redio kutoka nje ya nchi, Mh. Rais amesikia kilio chenu cha muda mrefu ameamua kuleta uwekezaji mkubwa wa kufanya usikivu Ngorongoro uwe bora,” amesema Biteko

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM (Loliondo Ngorongoro) kwenye kiwanja cha Kassim Majaliwa Majaliwa.