Rayvanny anyakua tuzo tano EAEA

0
379

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny, usiku wa kuamkia leo ameshinda Tuzo tano za East Africa Arts Entertainment Awards (EAEA) zilizotolewa nchini Kenya.

Tuzo alizoshinda ni Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki, Album Bora (EP) Afrika Mashariki, Mwandishi Bora wa nyimbo Afrika Mashariki, Best Lover Single Afrika Mashariki na Best Inspirational Single Afrika Mashariki.

Wasanii wengine walioshinda Tuzo hizo ni pamoja na Diamond Platnumz katika kipengele cha Hit-maker overall of the year ikiwa na nyimbo Shuu, Achii, My baby na Enjoy aliyoshirikishwa na Jux.

Mwingine ni Harmonize ambaye ameshinda Tuzo ya Overall Hit Single of the year Afrika Mashariki ambayo ni single Again.