Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewasili Loliondo mkoani Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM (Loliondo Ngorongoro) Aprili 15, 2024.
Dkt. Biteko amepokelewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Aisha Dachi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Stephen Kagaigai pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF,) Justina Mashiba.