Waziri Mkuu awasili Arusha

0
1000

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Arusha leo Aprili 11, 2024 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda tayari kwa kushiriki kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine.

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwaongoza Watanzania katika kumbukizi hiyo ya Hayati Sokoine kesho ljumaa itakayofanyika Monduli, Arusha.