Singida FG yahofia kipigo kutoka kwa Yanga

0
1377

Msemaji wa Singida Fountain Gate, Mussa Masanza amesema anahofia timu yake kupokea kipigo kutoka kwa Yanga kutokana na uwezo wa timu hiyo kwa sasa.

“Hakuna mtu anayetamani kukutana na Yanga… Tunasikitika kumkosa Thomas Ulimwengu, ila tunaamini dakika 90 ndio zitaongea,” amesema.

Masanza amesema hayo Jijini Mwanza wakati akizungumzia kuhusu maandalizi ya mechi baina yao na Yanga.