Mayele : Nitukane mimi, sio watoto wangu

0
1924

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele ameeleza kuchukizwa na kitendo cha watu wanaoweka jumbe za matusi kwenye ukurasa wake wa Instagram, na kwamba alikwazika zaidi siku walipofanya hivyo kwenye picha ya mwanaye aliyoichapisha.

Katika mahojiano na AzamTV, Mayele amesema matusi hayo yalipelekea baba yake mzazi kumpigia simu kuuliza mbona watu wanamshambulia mwanaye, ndipo Mayele akamjibu kwamba “nilikosea kucheza Tanzania.”

Amesema kuwa kama mtu anataka kumshambulia, amshambulie yeye na sio watoto wake kwa sababu wao hawachezi mpira, bali yeye ndiye anacheza.