Klabu ikidaiwa na mchezaji haishiriki ligi

0
531

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefungua ‘dirisha’ la klabu kuanza kuomba leseni kwa msimu wa 2024/2025 na kuweka wazi kwamba klabu yoyote itakayokuwa inadaiwa na mchezaji haitapata leseni kushiriki ligi.

Taarifa imefafanua kwamba usajili huo ni kwa ajili ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC, NBC Championship, First League na Ligi Kuu ya wanawake (TWPL). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, usajili utaanza rasmi April 15, 2024 hadi Mei 14, 2024.

Taarifa imesisitiza kwamba kwa klabu zitakazoshiriki mashindano ya CAF, kocha mkuu lazima awe na diploma A ya CAF na kocha msaidizi awe na diploma B ya CAF.