V8 yenye namba bandia yakamatwa ikisafirisha wahamiaji

0
558

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linawashikilia raia 17 wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila ya kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kutokuwa na vibali.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu amesema raia hao wa Ethiopia wamekamatwa katika kijiji cha Kiongozi wilayani Babati.

Amesema raia hao walikuwa wakisafirishwa kwa kutumia gari aina ya V8 VXR iliyowekwa namba bandia zinazosomeka kama STL 1964.

Kufuatia tukio hilo Kaimu Kamanda Mwakatundu amewaomba wananchi kushirikiani na Jeshi la Polisi kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa kutoa taarifa za watuhumiwa.