Kanisa Katoliki Matombo kutimiza miaka 125

0
481

Waumini wa Kanisa Katoliki Mtakatifu Paulo Matombo mkoani Morogoro wanatarajia kusheherehekea miaka 125 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Paulo Matombo, Octaviani Msimbe amesema Jubilei ya miaka 125 ya kanisa hilo itafanyika mwezi Oktoba mwaka huu kanisani hapo.Amesema wakati kanisa hilo likitimiza miaka 125 tangu kuanzishwa kwake, zaidi ya shilingi Milioni 200 zinahitajika kwa ajili ya kulifanyia ukarabati pamoja na ujenzi wa nyumba za Mapadre na Masista.

Paroko Msimbe amewaomba Watanzania wote kuchangia ukarabati wa kanisa hilo kutokana na baadhi ya miundombinu yake kuchakaa.