Simba yatoa pole ajali za mashabiki

0
787

Simba SC imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa ya ajali za mashabiki wake zilizotokea usiku wa kuamkia leo wakati wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kutazama mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Ajali ya kwanza ni ya mashabiki wa Tawi la Kiwira Rungwe la mkoani Mbeya ambayo imetokea eneo la Vigwaza mkoani Pwani, ambapo mtu mmoja amefariki dunia.

Ajali nyingine ni ya mashabiki wa Tawi la Wekundu wa Border kutoka Tunduma mkoani Songwe iliyotokea Doma mkoani Morogoro ambapo mtu mmoja ameumia.

Simba imesema viongozi wake wanaelekea eneo la Vigwaza kwa ajili ya kutoa msaada kwa waathirika na kwamba inatoa pole kwa wote walioathirika na ajali hizo.