Biteko mgeni rasmi sherehe Bomba la Mafuta

0
520

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ni mgeni rasmi kwenye sherehe za uzinduzi wa kiwanda cha kuweka mifumo ya kupasha na kutunza joto kwenye Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani, Tanga Tanzania.

Sherehe hizi zinarindima kwenye Kijiji cha Sojo wilayani Nzega, Tabora kinachopakana na Wilaya ya Kahama.

Pamoja na uzinduzi wa kiwanda hicho, pia utafanyika utiaji saini wa makabidhiano ya ardhi kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na EACOP pamoja na mkataba wa kuridhia kutumika kwa bandari ya Tanga katika utekelezaji wa mradi.

Endelea kufuatilia TBC Digital kwa taarifa za kina.