Samia aandika historia huduma za afya

0
333

Miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan ameweka historia kwenye sekta ya afya ambapo tangu uhuru Tanzania ilikuwa na mashine za MRI saba, lakini ndani ya miaka mitatu amenunua mashine sita na hivyo kuifanya Tanzania kuwa na mashine hizo 13.

Kwa mujibu wa miongozo ya afya, mashine hizi ambazo hutumika kupima na kugundua magonjwa mbalimbali kama vile uvimbe tumboni, kwenye ubongo, uti wa Mgongo na pingili za mgongo, hupatikana katika Hospitali za Rufaa za Kanda.

Katika hatua nyingine Rais Samia amewezesha kununuliwa kwa mashine mpya 32 za CT Scan, hivyo kuifanya nchi kuwa na mashine 45, kutoka mashine 13 zilizokuwepo tangu nchi kupata uhuru.

Mashine hizi za kiuchunguzi sasa zinapatikana kwenye hospitali zote za rufaa za mikoa, tofauti na awali ambapo baadhi ya wakazi wa mikoa, mfano Mtwara, iliwabidi kusafiri hadi Dar es Salaam kupata huduma hiyo, au wakazi wa Katavi waliolazimika kwenda Mbeya kupata huduma.

TBC Digital ipo bega kwa bega kukutembeza kwenye safari ya mafanikio ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani pamoja na kukuletea wasemayo wananchi kuhusu kiongozi wao.

MiakaMitatuYaRaisSamia #tbconline #tbcupdates #tbcdigital