Leo ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Upandaji Miti Kitaifa, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amepanda mti wa kumbukumbu katika Shule ya sekondari Same iliyopo mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Misitu Duniani na Upandaji Miti Kitaifa yamebeba kauli mbiu inayosema ‘Misitu na Ubunifu’.