Kiwanda chaunganisha simu elfu 40 Arusha

0
2074

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametembelea kiwanda cha TANZTECH kilichppo jijini Arusha kinachounganisha vifaa vya kielektroniki kama simu janja, vishikwambi na kompyuta

Katika ziara yake Waziri Nape ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa uwekezaji mkubwa walioufanya katika sekta ya mawasiliano ya simu.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho cha TANZTECH Gurveer Hans amesema kiwanda hicho ni cha kwanza nchini kinachoendeshwa kwa ushirikiano na Wachina ambao pia wamewekeza kwenye viwanda kama hivyo katika nchi za Uganda na Ethiopia.

Kwa sasa kiwanda hicho kimeanza kuunganisha simu janja elfu 40 kwa mwezi, vishkwambi elfu 30 kwa mwezi, kompyua mpakato elfu 15 na projekta elfu 10 kwa mwezi.

Waziri Nape ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa uwekezaji huo na pia kwa kuajiri wafanyakazi wazawa ambapo asilimia 90 ya wafanyakazi hao ni Wanawake.