CCM : Tunajivunia uongozi wa Rais Samia

0
237

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Emmanuel Nchimbi amesema Watanzania wanajivunia uwezo mkubwa wa kiuongozi aliouonesha Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake, ukijidhihirisha kwa namna anavyoiongoza nchi.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika unaoendelea nchini Zimbabwe Balozi Nchimbi amesema CCM pia inajivunia uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoendelea kuiongoza Serikali katika kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.

Ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuimarisha na kuboresha uhusiano wa nchi na vyama rafiki katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na kwamba anafuatilia mkutano huo wa 11 wa Makatibu Wakuu wa vyama hivyo kwa karibu.