Asali inayozalishwa mkoani Tabora imeshika nafasi ya pili kwa ubora kupitia mashindano ya ubora wa asali inayozalishwa Barani Afrika.
Hayo yameelezwa mkoani Dar es Salaam na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo alipokuwa akizungumzia mafanikio ya Wakala huo katika kipindi cha miaka.mitatu ya uongozi wa Rais Samia.Suluhu Hassan.
Amesema asali ya Tanzania hupimwa katika maabara za Kimataifa za Ithibati kila mwaka na kwa miaka yote imepata alama za juu kwa wastani wa 96/100.
Profesa Silayo amesema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Tanzania imeuza tani elfu 5.6 za asali nje ya nchi yenye thamani ya Dola Milioni 40 za Kimarekani.
“Masoko makubwa yako nchi za Umoja wa Ulaya, Uarabuni, Marekani, EAC na SADC,” Amesema Profesa Silayo.