Miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu amefanya kazi kubwa ya kukuza utalii hasa kuanzia kurekodi filamu ya Tanzania: The Royal Tour, kutangaza fursa za kitalii katika ziara zake za kimataifa pamoja na kualika wageni kutembelea Tanzania katika majukwaa mbalimbali.
Kutokana na jitihada hizo idadi ya watalii imeongezeka ambapo Tanzania imeweka rekodi ya kufikisha watalii kutoka nje milioni 1.8, idadi ambayo haijawahi kufikiwa katika historia ya Tanzania.
Aidha, jitihada hizo pia zimeiwezesha Tanzania kuwa nchi ya pili Afrika kwa ongezeko la watalii kwa mwaka 2023 pamoja na kuwa miongoni mwa nchi 10 duniani ambazo utalii wake umekuwa kwa kasi zaidi baada ya janga la UVIKO19.