Machi 19 mwaka huu, Rais Samia Suluhu anatimiza miaka mitatu madarakani, ambapo chini ya uongozi wake kuna viashiria mbalimbali vya kukua kwa uchumi, moja wapo ni fedha zilizopo katika mzunguko.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2021 wakati Rais Samia anaingia madarakani fedha zilizokuwa kwenye mzunguko zilikuwa shilingi trilioni 6.1, lakini katika miaka mitatu ya uongozi wake, zimeongezeka kwa shilingi trilioni 1.3, kufikia shilingi trilioni 7.4 mwaka 2023.
Ongezeko la mzunguko wa fedha huchangiwa na mambo mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa na utoaji huduma, usimamizi bora wa Sera ya Fedha, matumizi ya fedha kwa watu kuongezeka na kukua kwa biashara na uwekezaji.