Makamba atembelea Makaburi ya mauaji ya kimbari

0
325

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba, ametembelea Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali (Kigali Genocide Memorial) yaliyopo nchini Rwanda na kuweka shada la maua.

Akiwa kwenye Makumbusho hayo Waziri Makamba amewasihi wale wote wenye ushawishi mkubwa na nia njema ama ovu kwa nchi zao kutembelea makumbusho hayo ili kujifunza umuhimu wa umoja na athari chanya ama hasi zinazoweza kuletwa na matendo yao,

Takribani miili 2, 500 ya watu waliouawa katika mauaji hayo ya Kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 imezikwa hapo.

Waziri Makamba yupo nchini Rwanda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu inayolenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.