Kinana amtembelea Dkt. Mwinyi

0
224

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amemtembelea Makamu wa CCM, Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi siku chache baada ya mazishi ya baba yake, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi. Mzee Mwinyi alifariki dunia Februari 29, 2024, Dar es Salaam na kuzikwa Machi 2, 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.