Filamu ya Oppenheimer imeshinda tuzo saba katika tuzo za 96 za Oscar zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Machi 11, 2024 kwenye ukumbi wa Dolby Theatre uliopo Hollywood, Los Angeles nchini Marekani.
Tuzo ambazo Oppenheimer imeshinda ni
Best picture,
Best cinematography,
Best film editing,
Best original score,
Best directing – Christopher Nolan,
Best actor in a leading role, Cillian Murphy, na
Best actor in a supporting role – Robert Downey Jr.
Oppenheimer ni filamu ya kusisimua ya mwaka 2023 iliyoandikwa, kuongozwa na kutayarishwa na Christopher Nolan, na Cillian Murphy ameigiza kama J. Robert Oppenheimer, mwanasayansi wa silaha za atomiki wa Marekani aliyekuwa akifanya kazi katika mradi wa Manhattan wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.
Je, Umewahi kutazama filamu hiyo ya Oppenheimer au ndio unaenda kuisaka?.