Mgaya ateuliwa Mkuu wa chuo NIT

0
188

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Prosper Mgaya kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Anachukua nafasi ya Profesa Zacharia Manilwa ambaye amemaliza muda wake.