Watoto wanakufa kwa njaa Gaza – WHO

0
291

Watoto wanakufa kutokana na njaa Kaskazini mwa Gaza, Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema.

Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ziara za shirika hilo mwishoni mwa wiki katika hospitali za Al-Awda na Kamal Adwan ambazo ni za kwanza kufanywa tangu Oktoba mwaka jana, zimeonesha kuwa hali ya njaa ni kubwa na ya kutisha.

Katika chapisho la shirika hilo kwenye mitandao ya kijamii, Ghebreyesus amesema ukosefu wa chakula ni mkubwa na umesababisha vifo vya watoto 10 na wengi wana kiwango kikubwa cha utapiamlo huku majengo mengi ya hospitali yakiwa yameharibiwa.

Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza iliripoti siku ya Jumapili kwamba watoto wasiopungua 15 walikufa kutokana na utapiamlo na upungufu wa maji mwilini katika hospitali ya Kamal Adwan pekee.