Kwa nini leo, ‘Super Tuesday’ ni muhimu kwa Wamarekani

0
817

LEO Machi 5 maarufu “Super Tuesday, ni siku muhimu kwa Marekani kwani inaamua nani anakwenda kuchuana na Rais Joe Biden katika mbio za urais wa Marakeni kupitia chama cha upinzani cha Republican.

Ni kwamba, Donald Trump anawania tena urais wa Marekani, na leo kutapigwa kura zitakazoamua endapo atamshinda mpinzani wake, Nikki Haley, na kuwa mgombea mteule wa Chama cha Republican katika uchaguzi wa utakaofanyika Novemba 2024 au la.

Uchaguzi wa leo wa Republican utafanyika katika majimbo 15, yakiwemo yenye watu wengi zaidi ya California na Texas. Mpaka sasa Trump anaongoza akiwa na wajumbe 122 dhidi ya 24 wa Nikki Haley.

Upigaji kura utaendelea hadi Juni 2024 ikiwa Trump atachagua kusalia kwenye kinyang’anyiro hicho. Kila Trump anaposhinda kunamleta karibu na marudiano ya uchaguzi kati ya rais huyo wa zamani na Rais wa sasa, Joe Biden kutoka chama cha Demokrati.

Nikki Haley, balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, ndiye mpinzani pekee wa Trump aliyesalia baada ya Gavana wa Florida, Ron DeSantis kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono Trump.