Mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuzikwa leo jioni kijijini kwake Mangapwani mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kabla ya Maziko hayo, Mwili wa Mzee Mwinyi utapelekwa kwenye uwanja wa Amaan kwa ajili ya kuagwa na kisha kupelekwa katika Msikiti wa Zenjibar uliopo mkoa wa Mjini Magharibi kwa ajili ya kuswaliwa.
Kwa mujibu wa ratiba ya maziko ya Mzee Mwinyi, mwili wake utapitishwa kwenye mitaa kadhaa ya Kisiwa cha Unguja na kisha kupelekwa Mangapwani kwa ajili ya maziko.
Mzee Mwinyi amefariki dunia Februari 29, 2024 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka.99.