Wafunga barabara wakishinikiza iwekewe matuta

0
332

Wananchi wa Kijiji cha Tabu Hoteli kilichopo Kata ya Chigela wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro, wamelazimika kufunga kwa muda barabara kuu ya Morogoro- Dodoma wakishinikiza kuwekwa matuta ya kupunguza kasi katika eneo hilo. Hii ni baada ya mtoto wa miaka mitano aliyekuwa anatoka shule kugongwa na gari lililokuwa kasi na kufariki dunia papo hapo.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi hao wamesema matukio ya kugongwa watoto yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika eneo hilo la barabara.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabiri Makame amesemea utaratibu wa uwekeji alama za barabarani kwenye eneo hilo tayari zimeshafanyika na kwamba mkandarasi aliyepewa kazi hiyo tayari ameshafika wilayani Gairo.