Takribani Wapalestina 112 wameuawa na wengine 760 kujeruhiwa wakati wakiwa kwenye mchakato wa kusaka msaada hususani wa chakula katika ukanda wa Gaza.
Umati wa watu ulijikusanya kwenye msafara wa malori yaliyokuwa kwenye barabara ya kusini-magharibi mwa Jiji la Gaza, mbele ya mizinga ya Israel wakiamini watapata msaada kutoka kwenye malori hayo.
Jeshi la Israel limesema vifaru vilifyatua risasi za onyo lakini havikushambulia msafara huo. Lakini baadhi ya Wapalestina wameiambia BBC kwamba wanajeshi wa Israel walifyatulia risasi moja kwa moja wakiwalenga raia hao bila huruma.