Serikali imedhamiria kuyafanya makazi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyoko Mwitongo, Butiama mkoani Mara kuwa kituo cha utalii.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Muhumba, wilayani Butiama, akiwa njiani kuelekea Mugumu, Serengeti kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara.
Amemuagiza mkuu wa wilaya ya Butiama, Moses Kaegele atembelee eneo hilo, akague na kuangalia mapungufu yaliyopo ili Serikali iweze kuyafanyia kazi.
Akiwa Mwitongo Waziri Mkuu Majaliwa alipata fursa ya kuwasalimia wanafamilia wa Hayati Baba wa Taifa na kuweka shada la maua kwenye kaburi lake.