Yanga: Tunaitaka fainali ya Ligi ya Mabingwa

0
487

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema lengo lao baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kufika hatua ya fainali ya mashindano hayo.

Kamwe amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Amewasisitiza mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuiunga mkono na kujitokeza uwanjani kama ilivyokuwa kwenye mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad.

“Rais wa nchi, Samia Suluhu alisema Yanga SC imefurahisha nchi, hivyo ni wajibu wetu kuendelea kufurahisha nchi,” amesema Kamwe.

Yanga inaondoka nchini leo kwenda Misri katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Al Ahly ambapo timu hizo kutoka Kundi D tayari zimefuzu hatua ya robo fainali.