Miradi 526 imesajiliwa nchini mwaka 2023

0
676

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) miradi 526 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.7 ilisajiliwa nchini kwa mwaka 2023, ikilinganishwa na miradi 256 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.7 iliyosajiliwa mwaka 2021.

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua Jukwaa la Kodi na Uwekezaji la mwaka 2024 kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kuwa miradi hiyo ipo katika sekta mbalimbali zikiwemo uzalishaji, ujenzi wa majengo ya biashara, usafirishaji na sekta ya kilimo.