Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Shariff Ali Shariff kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).
Uteuzi huo umefanyika leo na Shariff ataapishwa kesho Februari 22, 2024 katika ukumbi wa Baraza la Mapinduzi, Ikulu, Zanzibar, saa 8:00 mchana.