Rais Magufuli achangia ujenzi wa Msikiti Kyela

0
381

Rais John Magufuli ametoa Shilingi Milioni Tano kwa waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa msikiti huo, hatua iliyoungwa mkono pia na Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson aliyechangia Shilingi Milioni Mbili, huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kyela Dkt Harrison Mwakyembe akichangia Shilingi Laki Tano.

Watu wengine mbalimbali pamoja na maafisa wa serikali waliofuatana na Rais Magufuli katika ziara yake wilayani Kyela nao wamechangia ujenzi wa msikiti huo.

Zaidi ya Shilingi Milioni Ishirini zimepatikana.