Mwanaume mwenye umri wa miaka 42 anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya ndugu watatu nchini Hispania, anadaiwa tena kumuua mahabusu mwenzake gerezani anakoshikiliwa, ripoti zimesema.
Mtuhumiwa huyo aliyetambuliwa kama Dilawar Hussain F.C., alihamishiwa katika gereza la Estremera, lililoko nje kidogo ya Jiji la Madrid mwezi uliopita.
Inadaiwa kwamba mtuhumiwa huyo alikiri kuwaua dada wawili na kaka yao katika mji wa Morata de Tajuña.
Mapema leo, kengele imegonga katika gereza hilo baada ya kugundulika kwamba kuna mahabusu alikuwa amekufa katika chumba cha mahabusu na uchunguzi umeonesha kwamba ameuawa.