Lindi na Mtwara kupata umeme wa uhakika

0
259

Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba
amesema lengo la Serikali ni kuimarisha na kuongeza uzalishaji wa umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mhandishi Mramba ametoa kauli hiyo katika kijiji cha Hiyari halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakati wa mapokezi ya mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara mwaka 2023 na kuagiza mikoa hiyo ipate umeme wa uhakika.

Mtambo huo wa kuzalisha umeme uliopokelewa mkoani Mtwara ni mkubwa na wa kisasa na unaitwa TM16 ambao unafanyakazi saa elfu 25 bila kufanyiwa matengenezo.

Utakuwa unahitaji matengenezo madogo madogo na utazalisha umeme ambao utawashwa Machi 31, 2024 na kuwa suluhisho la kuzalisha umeme wa uhakika kwa mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara.