Apatiwa ramani aliyoidai miaka 4 baada ya agizo la Makonda

0
200

Katibu wa NEC, Itikadi, Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda amefanikisha kupatiwa ramani Mwanamke mmoja wa Manispaa ya Iringa aliyeifuatilia ramani hiyo kwa miaka minne ofisi ya ardhi bila mafanikio.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Makonda alilolitoa jana Februari 08, 2024 baada ya Mwanamke huyo kumlilia na kusema licha ya kulipa shilingi Milioni 3 bado hajapewa ramani yake.

Ndipo Makonda aliwataka maafisa Ardhi wa Manispaa ya Iringa kumpatia Mwanamke huyo ramani yake ndani ya saa 14.