Rais Mwinyi ataka Wazee wasaidiwe zaidi

0
185

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Wazee Wanahitaji msaada zaidi hasa katika kuimarisha afya zao.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na wawakilishi wa Shirika la AARP la nchini Marekani, linalojihusisha kustawisha maisha ya Wazee waliomtembelea Ikulu, Zanzibar.

Amelitaka shirika hilo kuzungumza na mashirika mengine ya Kimataifa na kuangalia namna ya kuwasaidia Wazee kwenye masuala ya Afya.

Rais Mwinyi amesema kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeimarisha pensheni kwa Wazee kwa kuwaongezea malipo, na inafikiria kushusha umri wa kuwalipa pensheni kutoka miaka 70 hadi 60.