Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema ni muhimu kwa Wanasiasa nchini kuyaishi maisha ya demokrasia kama wanavyoitangaza majukwaani ili kuenzi utawala bora uliokuwepo hata kabla na baada ya ukoloni.
Dkt. Rioba ametoa kauli hiyo alipokuwa akiwasilisha
mada kwa Wakufunzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kuhusu dhima ya Shirika la Utangazaji Tanzania katika muktadha wa Demokrasia.
Ameeleza kuwa TBC ni chombo kinachotumika kutoa elimu sahihi ya Usalama wa Taifa kupitia vipindi vyake kutokana na historia na matukio ya viongozi mbalimbali wa Taifa.
Wakufunzi hao kutoka NDC wametembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania zilizopo Dar es Salaam kwa lengo la kujiionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo.